KATIBU Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania(TFF), Angetile Osiah
amejiondoa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Yanga na
kusema, uamuzi wake haukusukumwa na taswira ya mgogoro wa uongozi ndani
ya klabu hiyo.
Karibu wiki moja iliyopita, Mwenyekiti wa Yanga
Llyod Nchunga alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya takribani mwezi
mzima wa shinikizo la kumtaka kuchukua uamuzi huo toka kwa wanachama wa
klabu hiyo.
Shinikizo la kumtaka Nchunga kuachia nafasi hiyo,
kulitanguliwa na wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo
kujiuzulu nafasi zao na kubaki wanne toka 12.
Wakati akijiuzulu, Nchunga alisema amefikia hatua hiyo ili kuepuka kuwa chanzo cha ukosefu wa amani ndani ya Yanga.
Akiongea
jana jijini Dar es Salaam, Osiah alisema uamuzi huo umekuwa wa lazima
kwa vile siyo rahisi kwake kutumikia kofia mbili kwa wakati mmoja.
"Majukumu
yamekuwa mengi, siyo rahisi tena kwangu kutumikia nafasi mbili kwa
wakati mmoja, lakini ni vizuri pia nikasisitiza kwamba, uamuzi wangu
hauhusiani na kinachoendelea Yanga," alisema Osiah.
Bosi huyo wa
TFF alisema, kujiondoa kwake kwenye kamati hiyo ya uchaguzi hakujabeba
tafsiri kwamba, hatahusika tena majukumu ya kawaida ndani ya klabu hiyo.
"Nitaendelea
kuwa mwanachama halali wa Yanga kwa vile nina kadi iliyo hai. Nitakuwa
tayari wakati wowote kushirikiana na uongozi wa Yanga kama watahitaji
msaada wangu," alisema Osiah.
Alisema tayari amewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa Katibu mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa.
"Kanuni ya uchaguzi ya Yanga kifungu cha 5 zinaruhusu kujipunguzia majukumu endapo sababu ya kufanya hivyo itakuwapo, hivyo amezingatia na kuheshimu kanuni nikiwa kama mpenda michezo," alisema
"Kanuni ya uchaguzi ya Yanga kifungu cha 5 zinaruhusu kujipunguzia majukumu endapo sababu ya kufanya hivyo itakuwapo, hivyo amezingatia na kuheshimu kanuni nikiwa kama mpenda michezo," alisema
Chanzo:- Mwananchi
Post a Comment