
Nyaraka hizo zimechapishwa kwenye mtandao na kitengo cha utafiti katika chuo cha kijeshi cha West Point, nchini Marekani.
Maelezo
na nyaraka 17 zilizotolewa wazi kwa umma ni pamoja na barua na
mawasiliano mengineyo ya elektroniki ambayo kwa jumla ni kurasa mia moja
na sabini na tano, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2006 hadi mwezi Aprili
mwaka jana, muda mfupi kabla ya Osama bin Laden kuuawa.
Watafiti wa jeshi la Marekani, ambao
walishuhudia nyaraka hizo kutolewa kwa umma, wanaelezea kwamba
zinaonyesha kiongozi huyo wa Al Qaeda tayari alikuwa ameanza kuudhika
kutokana na muelekeo wa makundi ya Jihad.
Alikuwa anafikiria uwezekano wa muungano wa
Waarabu kama jambo linalowezekana, lakini akiwashauri wafuasi wake
kuangazia lengo lao la kuishambulia Marekani, na akielezea kwamba
kimsingi hilo ndio lengo lao kuu.
Katika barua moja, Bin Laden anapendekeza
kuangazia kuzishambulia ndege zinazomsafirisha Rais Obama katika ziara
zake nchini Afghanistan, na kwamba makamu wa Rais Joe Biden atashtuka
kufuatia tukio hilo na kushindwa kuiongoza nchi.
إرسال تعليق