Jaji Munuo achaguliwa Rais wa majaji duniani


na Irene Mark



JAJI Eusebia Munuo wa Mahakama ya Rufani Tanzania, amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili kutoka nchini Uingereza kulikofanyika uchaguzi huo, Jaji Munuo alisema nafasi hiyo inaonesha namna Tanzania inavyoheshimika ulimwenguni.
“Nimeanza kuitumikia nafasi ya urais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani Mei 6, mwaka huu na nitadumu kwa miaka miwili. Tulikwenda majaji na mahakimu 38 kwenye uchaguzi huo,” alisema Jaji Munuo.
Alisema taifa litaingiza watalii wakati wa mkutano wa chama hicho kidunia utakaofanyika hapa nchini Mei 4 hadi 6 mwaka 2014 huku akisisitiza kwamba licha ya udogo na umaskini wa taifa hili linaheshimika duniani.
Jaji Munuo aliyeongozana na baadhi ya majaji wanawake kwenye mkutano huo, alisema kesi zote zitakazotolewa uamuzi zitaingizwa kwenye mtandao, hivyo dunia kuona na kutambua kinachoendelea.
“Tumefanya vema katika kuelimisha mahakimu na majaji wetu kusimamia haki za binadamu na kuleta usawa katika jamii… tumezunguka mikoa mbalimbali na mwezi ujao tutatoa elimu hiyo pia kwa wabunge,” alisisitiza jaji huyo.
Alisema kaulimbiu ya mkutano uliomweka madarakani ambao ulihudhuriwa na majaji zaidi ya 600 ni ‘Kuwa salama na afya njema’.
Kwa habari zaidi ingia hapa:- http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=35752

Post a Comment

أحدث أقدم