JK: Serikali italinda ardhi ya wakulima wadogo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa Afrika wakiwa katika mdahalo wa taasis ya kilimo ya GroAfrica
kwenye jengo la Makao Makuu Mapya ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia leo, Mdahalo huo umefanyika kingoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Kimataifa kwa Afrika.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa
miradi mikubwa ya kilimo ya kibiashara nchini itatekelezwa kwa shabaha
mbili kubwa - ambazo ni kuwatoa wakulima katika umasikini na kulinda
miliki ya ardhi yao.
Aidha,
Rais Kikwete ameambiwa kuwa Marekani inataka kuhakikisha kuwa Mradi wa
Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania – Southern
Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) unakuwa ni mfano
unaong’ara wa uendelezaji kilimo katika Bara la Afrika.
Akizungumza
na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Dkt.
Rajiv Shah kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia, Rais
Kikwete amesema kuwa shahaba kuu zaidi ya miradi kama SAGCOT ni kuwatoa
wakulima wa Tanzania katika umasikini katika kipindi kifupi na kulinda
miliki ya ardhi yao.
Rais
Kikwete na Dkt. Shah wako mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), Kanda ya Afrika, ulioanza
leo, Jumatano, Mei 9, 2012.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumzia hofu ya baadhi ya watu kuwa miradi mkubwa
ya kilimo nchini itachukua ardhi ya wakulima wadogo ili iweze
kufanikiwa. “Nia na madhumuni ya miradi mikubwa ya kilimo nchini siyo
kuwapora wakulima wetu ardhi yao. Hasha. Nia yetu ni kuwasaidia ili
wakue na watoke kwenye hali ya kilimo cha kujikimu na kuingia katika
kilimo cha biashara.”
Rais
amesema kuwa wakulima wakubwa watapewa ardhi tu pale ambako iko ardhi
ya kutosha na hata baada ya kupewa ardhi watatakiwa kuwasaidia wakulima
wadogo wanaokuwa wanaishi jirani na shamba la wakulima hao wakubwa.
“Tutawapa ardhi kubwa wakulima wakubwa pale ambako iko ardhi ya kutosha. Na hata baada ya kuwa tumepewa ardhi hiyo, wakulima
hao wakubwa watatakiwa kuwasaidia na kushirikiana na wakulima wadogo.
Hii ndiyo namna pekee ya kuwasaidia wakulima wetu kuondokana na
umasikini,” amesema Rais Kikwete.
Naye
Dkt. Shah amemwambia Rais Kikwete kuwa Marekani imedhamiria kuhakikisha
kuwa SAGCOT unakuwa mfano wa miradi ya mfano na inayong’ara katika
Afrika. USAID ni moja ya mashirika ya kimataifa ambayo inashirikiana na
Serikali katika kuendeleza mradi huo.
Dkt.
Shah pia amemweleza Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Nchi
Tajiri na Zenye Viwanda (G-8) ambao umepangwa kufanyika Marekani kuanzia
wiki ijayo. Rais Kikwete ni Waziri Mkuu wa Ethiopia, Bwana Meles Zenawi
ni miongoni mwa viongozi wane wa Afrika walioalikwa na Rais Barack
Obama wa Marekani kuhudhuria mkutano huo.
Katika
mkutano mwingine, Mtendaji Mkuu wa Benki ya HSBC, Bwana Andrew Dell
amemwambia Rais Kikwete kuwa benki yake iko tayari kuiwezesha Tanzania
kukopa fedha nyingi ya ujenzi wa miundombinu kwa mpango wa Sovereign
Bond badala ya kutumia fedha za kodi kujenga miundombinu ambayo inaweza
kujengwa kwa urahisi na kwa kutumia fedha ya benki hiyo.
Rais
Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na wakurugenzi wa Kampuni
ya MSP Steel and Power Limited ya India, Mabwana Manish Agrawal na
Pranay Agranal ambao wanataka kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.
Rais
amewakaribisha wakurugenzi hao kuwekeza katika uchumi wa Tanzania
akisisitiza kuwa Tanzania bado unahitaji wawezekezaji kwa wingi na
katika sekta zote

إرسال تعليق