KOCHA JUVENTUS AKAMATWA NA POLISI KWA KUPANGA MATOKEO, KAMBI YA ITALIA EURO 2012 YAVAMIWA NAHODHA wa Lazio amekamatwa na polisi kwa uchunguzi wa kupanga matokeo mchezoni.
Kiungo Stefano
Mauri, mwenye umri wa miaka 32, alishikiliwa kwa pamoja na kiungo wa
zamani wa Genoa, Omar Milanetto, polisi ilisema.
Kocha wa Juventus, Antonio Conte, ambaye ameiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Serie A katika msimu wake wa kwanza kazini, ni miongoni mwa waliohojiwa na polisi.
Maofisa wa
Polisi walitembelea pia kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Euro 2012
kumuhoji beki Domenico Criscito, mwenye umri wa miaka 25.
Polisi
walipekua nyumba zaidi ya 30, zikiwemo za wachezaji, makocha na viongozi
wa klabu za Serie A, Serie B na madaraja ya chini zaidi.
Polisi
ilisema Conte alifanyiwa uchunguzi juu ya shaka ya kushiriki mchezo
mchafu wa kupanga matokeo mchezoni kati ya klabu yake ya awali, Siena na
Novara, Aprili mwaka 2011. Watu wengine watano walikamatwa pia nchini Hungary kwa kuhisiwa kuwa sehemu ya mchezo huo mchafu, unaopigwa vita kali.
إرسال تعليق