MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AFUNGA AWAMU YA KWANZA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, MKOANI TABORA LEO.


Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunga kitambaa juu ya ramani ya Tanzania, kuashiria kufunga Awamu ya
kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9,
2012, Mkoani Tabora. Zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi
inatarajia kuanza Tarehe 26 Mwezi Agosti, mwaka huu.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuashiria kuhakiki Ramani ya iliyoandaliwa kwa zoezi
la kuhesabu Sensa ya watu linalotarajia kuanza Tarehe 26 Mwezi Agosti,
mwaka huu, wakati alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya
Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, mkoani Tabora.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa
Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya
kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi
iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora.


Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza
ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012
katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.

Makamu
akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya
kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9,
2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin
Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
إرسال تعليق