Mapigano yalizuka jana jioni wakati wanajeshi wa
rais wa zamani Amadou Toumani Toure walipojaribu kudhibiti televisheni
ya serikali kutoka kwa wanajeshi waliotwaa udhibiti wa kituo hicho
katika mapinduzi, mwezi Marchi.
Viongozi wa mapinduzi hayo wamesema wanajeshi
hao wa rais wa zamani pia walijaribu kudhibiti uwanja wa ndege, ili
kujiandaa kuwasili kwa jeshi la mataifa ya magharibi, ambalo madhumani
yake ni kurudisha utawala wa kiraia. Mpango huo tayari umekataliwa na
viongozi hao wa mapinduzi.
Walioshuhudia wanasema kufuatia mapigano hayo,
sasa mitaa ya mji wa Bamako haina watu na kwamba umeme umekatwa katika
maeneo mengi.
Televisheni ya serikali imekuwa ikipeperusha vipindi badala ya habari.
Baadhi ya ripoti zinaashiria kuwa vurugu hizo
zilichochewa na jaribio la kutaka kumkamata afisa wa zamani ya rais
Toumani Toure, aliyemsaidia kutoroka wakati wa mapinduzi.
Chanzo:- BBC Swahili
إرسال تعليق