Msaidizi wa Mahalu akana kuisababishia serikali hasara
Profesa Costa Mahalu
Mshatakiwa
wa pili na aliyekuwa Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini
Italia, Grace Martin (50), amekanusha kuisababishia serikali hasara ya
Euro 2,065,827.60 katika mkataba wa ununuzi wa jengo la ubalozi.Hata
hivyo, Grace aliiambia Mahakama jana kuwa alishiriki katika mchakato wa
kupatikana mpaka kutia saini kwa mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la
ubalozi huo.
Kadhalika,
aludai kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kutoa kibali cha kufanyika mchakato wa kupata
jengo la kudumu la ubalozi nchini humo. Grace
ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi alitoa madai hayo jana
wakati akitoa utetezi wake huku akiongozwa na wakili wa utetezi,
Cathbert Tenga, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Illivin Mgeta, anayesikiliza kesi
hiyo.
Alidai
kuwa aliyekuwa balozi wakati huo, Profesa Costa Mahalu (63),
alistahili shukrani kwa kazi nzuri aliyoifanyia serikali na sio mashtaka
yanayomkabili. Alidai
kuwa aliyekuwa Mhasibu wa ubalozi huo, Prosper Migwano, ambaye
alihusika na utaratibu wote wa kutafuta mpaka kupokea nakala ya risiti
za malipo ya jengo hilo, alifunguliwa mashitaka pamoja na wao, lakini
anashangaa upande wa Jamhuri ulimfutia mashitaka na kumtumia kama
shahidi kwa upande wa mashtaka dhidi yao.
”Nashangaa
upande wa mashitaka kwamba aliyekuwa mtumishi na mhusika katika
mchakato huu tulishtakiwa naye mahakamani hapa, lakini sijui ni kwa
sababu zipi walimfutia mashtaka ambapo alikana kufahamu suala la
masharti ya mmiliki wa jengo hilo kwa kuandikiana naye mikataba
miwili...
Kitu
cha kushangaza zaidi Jamhuri walimtumia kama shahidi na alikana
kufahamu mikataba hiyo,” alidai Martin. Aidha, alidai kuwa mashtaka sita
yanayomkabili sio ya kweli na kwamba hakuna ushahidi uliothibitisha
tuhuma dhidi yake.
Jana
upande wa utetezi ulifunga ushahidi wake baada ya mashahidi watatu,
Grace, Profesa Mahalu na aliyekuwa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kutoa
ushahidi dhidi ya tuhuma hizo. Hakimu Mgeta alisema pande zote mbili
zitakabidhiwa mwenendo wa kesi Mei 16, mwaka huu ili ziweze kuandaa hoja
za kama washitakiwa watiwe hatiani au la.
Habari na - NA HELLEN MWANGO
CHANZO: NIPASHE
إرسال تعليق