
Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amesema wizara hiyo
inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo suala la wakimbizi,
uwingi wa wafungwa magerezani na utengenezwaji wa vitambulisho vya
taifa.
Alisema
hayo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi ofisi waziri mpya wa
wizara hiyo, Dk. Emmanuel Nchimbi, hivyo akamtaka akabiliane na
changamoto hizo.
Nahodha alisema wizara hiyo inakabiliwa na changamoto ya
kuwarudisha wakimbizi 37,000 wa Burundi waliohifadhiwa nchini.
kuwarudisha wakimbizi 37,000 wa Burundi waliohifadhiwa nchini.
“Wakimbizi
hao walitakiwa kurudishwa nchini kwao tangia Aprili 1, mwaka huu, hivyo
ni jukumu la wizara yako kutekeleza kazi hiyo niliyoiachia katikati,”
alisema Nahodha. Alisema wakimbizi 67,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC) hawatarudishwa kwao kutokana na hali ya amani katika nchi
kutokuwa ya kuridhisha.
Aliongeza
kuwa msongamano wa wafungwa magerezani ni moja ya changamoto
inayoikabili wizara hiyo, na kiliundwa kikosi kazi cha kufatilia kesi
zisizokuwa za msingi na kuzifuta kesi hizo ili watuhumiwa waachiwe huru.
“Ni
jukumu lako ni kuendeleza kazi tulioiachia katikati ya kuhakikisha
msongamano wa wafungwa magerezani unakwisha na kesi zisizokuwa na
ushahidi zinafutwa na watuhumiwa wanaachiwa huru,” alisema.
Nahodha
ambaye amehamishiwa Wizara ya Ulinzi na JKT, alisema, sula la
kutengeneza vitambulisho vya taifa ni moja ya changamoto inayoikabili
wizara hiyo na mpaka sasa wafanyakazi wa serikali 290,000 kutoka bara na
visiwani wameshaandikishwa, hivyo ni jukumu la wizara hiyo kuendeleza
kazi hiyo.
Kwa
upande wake Dk. Nchimbi alisema atajitaidi kuzikabili changamoto hizo
na kutoa wito kuwa vyombo vya dola viendelee kueshimiwa na umma.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق