Mkuu wa uchunguzi wa malalamiko(Ombudsman) nchini
Burundi, Mohamed Rukara, amegundua njama ya kumuua, kwa mujibu wa
msemaji wake.

Mauwaji yazidi Burundi
"ni hao wanaoiba fedha za umma," amesema Jerome Ndiho, bila kutaja majina.
Kama
mchunguzi huru,Bw.Rukara hufanya upelelezi juu ya madai yoyote
yanayofanywa na maofisa wa serikali, ikiwa ni pamoja na ''njama za
mauwaji ya raia''.
Makundi ya nchini humo yanadai kua serikali ya
Burundi inawakinga watu wanaoshiriki rushwa na imeshindwa kukabiliana na
ghasia zinazochochewa kisiasa.
'vitisho vya kuua'
Burundi bado inapitia kipindi cha ukarabati wake
kifikra na kitaifa kufuatia vita vya miaka 12 ya wenyewe iliyomalizika
mwaka 2005 -kisha ghasia za kisiasa zikafuata kufuatia uchaguzi ambao
haukuridhisha baadhi ya raia mwaka 2010.
Kundi la kupigania haki APRODH, limeandika mauwaji yasiyopungua 160 mwaka huu, yanayolaumiwa kufanywa na makundi ya wanausalam.

Viongozi wakubaliana
Mapema mwezi huu, ripoti ya kundi la Human
Rights Watch ilidokezea kila ilichokielezea kua 'kulipiza kisasi'' kwa
watu waliosababisha mgawanyiko wa kisiasa kutoka pande zote mbili.
Bwana Rukara amesema kua endapo watauawa,
ameomba asizikwe hadi Madaktari waifanyie uchunguzi maiti yake
kuhakikisha kilichosababisha kifo chake.
Shirika lenye makao yake mjini New York, huma
rights watch, linadai kua lilikataliwa kufanya makutano wa wandishi wa
habari mjini Bujumbura kuhusu ripoti yao.
Hata hivyo wakuu wa nchi wamejibu madai hayo
kama uzushi uliokithiri na kulaumu mauwaji juu ya makundi ya majangili
wenye silaha.
Bw.Rukara aliteuliwa kama mchunguzi(ombudsman)
wa kwanza nchini humo mapema mnamo mwaka 2011 kufuatia uteuzi uliofanywa
na bunge- takriban miaka kumi baada ya bunge hilo kuundwa chini ya
mapatano ya kwanza ya amani.
Inakadiriwa kua vita vya wenyewe kwa wenyewe
baina ya makabila ya Watutsi na Wahutu nchini Burundi viomesababisha
vifo vya hadi watu 30,000
Mzozo huo ulimalizika rasmi mwaka 2005 kwa
mapatano ya amani yaliyofuatiwa na kuchaguliwa kwa Bw.Pierre Nkurunziza
kama Rais wa nchi hio.
Kundi la mwisho la waasi lilisalimu amri mnamo
mwaka 2009 lakini mashambulizi ya hapa na pale yanazidi kutokea na
kusababisha baadhi ya raia wa nchi hio kukimbilia uhamishoni.
Chanzo:- BBC Swahili
Post a Comment