Picha Primo-Pascal Rudahigwa
Wakimbizi kutoka Congo wakiwa katika kambi ya Nkamira Transit nchini Rwanda
Raia wengi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanakimbia mapigano katika maeneo yao na kuelekea katika nchi jirani ya Rwanda.
Mkazi mmoja katika eneo la mashariki ya DRC ambako mapigano hivi sasa
yanaendelea, Annie Kabeja mwenye umri wa miaka 34 alisema wakati milio
ya risasi iliposikika katika eneo analoishi, aliungana na wimbi la
maelfu ya wakongo na kuondoka katika eneo ambapo alitembea kwa muda wa
siku mbili akiwa na mtoto wake hadi kuingia nchini Rwanda.
Bi.Kabera akiwa na mtoto wake mdogo mgongoni, alisubiri kwenye mstari
mrefu pamoja na wakongo wengine kwenye kambi ya wakimbizi ya Nkamita
Transit kupokea mgao wa chakula na mahitaji mengine ya msingi.
“Tulisikia milio ya risasi na milipuko. Tulikuwa hatuna uamuzi wa
kufanya isipokuwa kukimbia kutoka eneo hilo hadi eneo jingine na baada
ya kuwasili nchini Rwanda, hatukuweza kulala, risasi zilikuwa zikiruka
kila mahali.”
Mapigani huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC
yamezidi baada ya darzeni ya wanajeshi waasi siku ya Jumatatu kuunda
kundi jipya katika eneo kubwa ambalo waasi wengi walianzia huko.
Kundi hilo jipya liliundwa na wanajeshi waasi wanaojiita March 23,
ikiwa ni tarehe katika mkataba wa amani wa mwaka 2009 uliotiwa saini na
makundi ya uasi na serikali ya Congo. Kundi hilo linaongozwa na Kanali
ambaye zamani alikuwa chini ya Bosco Ntaganda, mbabe wa kivita wa zamani
ambaye aliingia katika jeshi la Congo chini ya mkataba wa amani licha
ya kutafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.
Msemaji wa jeshi la Congo, Kanali Sylvain Ekenge aliliita kundi jipya
ni ‘bandia’ lakini mapambano kati yao na jeshi la Congo yaliendelea kwa
siku kadhaa katika mkoa wa Masisi uliopo Kivu Kaskazini.
Rwanda kwa kawaida hutumia sehemu katika milima ya Rwanda, kuwakaribisha kwa muda wakimbizi kutoka Congo.
Straton Kamanzi meneja wa kambi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa
alisema kambi hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua wakimbizi 4,000 lakini
hivi sasa ina nyumba 7,000. Wanawake, wasichana na watoto wadogo
wanalala chini pamoja kwenye makazi ya muda.
Richard Ndaula ambaye anafanya kazi na shirika la kuhudumia wakimbizi
la Umoja wa Mataifa alisema kati ya watu 250 na 300 wanajitokeza kwenye
kambi hiyo iliyopo karibu na mpaka na Congo kila siku.
Chanzo:- http://www.voanews.com
Post a Comment