Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amemsifu msaidizi
wake katika klabu, Pat Rice, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu,
baada ya miaka 44 akiwa na 'Gunners'.
Mrithi wake atakuwa ni mlinzi wa zamani wa
Arsenal, Steve Bould. Rice, ambaye aliichezea Arsenal katika mechi zaidi
ya 500, alijiunga na wafanyikazi wa klabu ya Arsenal mwaka 1996, wakati
Mfaransa Arsene Wenger alijiunga na klabu kama meneja.
Kama meneja msaidizi, Rice aliisaidia Arsenal
kufanikiwa kupata ushindi wa ligi ya Premier mara tatu, na mara nne
kulitwaa Kombe la FA.
Meneja Wenger amesema ni vigumu kukadiria kazi
aliyoifanya Rice, na kuelezea kwamba ni jambo la "huzuni, huzuni, huzuni
sana, na binafsi namshukuru kwa mchango wake katika kunisaidia wakati
wangu na ningependa anisamehe kwa baadhi ya shida alizozipata katika
kipindi alichokuwa chini yangu, lakini alikuwa ni msaidizi mwaminufu
sana, na ninamshukuru kwa kuwa kando yangu kwa muda mrefu hivyo".
Post a Comment