Di Mateo ahakikishiwa kujadili Chelsea

Di Matteo
Kocha msaidizi wa Chelsea Roberto Di Matteo amehakikishiwa leo kuwa uwamuzi juu ya nafasi yake katika klabu hiyo utafanywa baada ya fainali ya Klabu bingwa.
Kuna tetesi kuwa Mkufunzi huyo wa muda amekua na unyonge wa kiasi akihisi kuwa Klabu hiyo ina mipango ya kumpokonya wadhifa wa kuwa Meneja wake na badala yake wamtafute mtu mwingine, hata ikiwa matokeo ya mechi dhidi ya Bayern Munich yatakua mazuri.
Lakini akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa ushirika wa klabu hiyo na timu ya magari ya mbio za Langalanga ya Sauber, Mkurugenzi mtendaji Ron Gourlay ameliambia shirika la habari Press Association kuwa, Klabu hiyo ina imani kubwa na Kocha huyo tangu ajiunge nao kama meneja wa muda na kwamba watafanya tathmini yao mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, Gourlay alishindwa kujibu kama Di Matteo amefanya kazi ya kutosha kuwekwa kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya Meneja wa klabu.
Hata kabla ya kufuzu kushiriki fainali ya Ligi ya mabingwa, mashabiki wengi walimuunga mkono Di Mateo achaguliwe kumrithi Andre Villas Boas.
Licha ya imani zote hizo, endapo Di Mateo atashindwa kuwika mjini Muinich,basi Abramovich ataitumia kama sababu ya kumuondoa Di Mateo ambaye atakua ameshindwa kuipandisha Chelsea kutoka nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Premiership na hivyo kukosa michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya mwakani.

Post a Comment

Previous Post Next Post