Yaya Toure ataka City iwe bora duniani

Yaya Toure amesema kuwa anataka kuisadia klabu yake ya Manchester City iwe klabu bora duniani.
Mcheza kiungo huyo amekua kiini cha klabu hiyo msimu huu, klabu ambayo wikendi hii inadhamiria kushinda kombe la Ligi ya Premier ya England.
Yaya amesema kuwa, sababu iliyonileta hapa ni kuisadia timu.......kusaidia katika kuiendesha mbele na kuifanya iwe kubwa kuliko zote duniani.
Yaya Toure
Yaya Toure
City inaipokea QPR siku ya Jumapili na ikishinda mechi hiyo wakati Manchester United ikishindwa kushinda Sunderland kwa angalau mabao kumi basi City itatawazwa bingwa wa msimu wa mwaka 2011/2012.
Alipoulizwa kama ameanza kuhisi shinikizo za pambano hilo la mwisho, Toure aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 24, alijibu hapana, kwa sababu nina uzoefu. Nimeisha shiriki michuano kama hii na kushinda vikombe kadhaa.
Toure, alikua na klabu ya Barcelona iliyoshinda vikombe sita vya nchini na nje ya nchi mwaka 2009 na amekua kishawishi kikubwa msimu huu kwa Manchester city.

Post a Comment

Previous Post Next Post