Yaya Toure amesema kuwa anataka kuisadia klabu yake ya Manchester City iwe klabu bora duniani.
Mcheza kiungo huyo amekua kiini cha klabu hiyo
msimu huu, klabu ambayo wikendi hii inadhamiria kushinda kombe la Ligi
ya Premier ya England.
Yaya
amesema kuwa, sababu iliyonileta hapa ni kuisadia timu.......kusaidia
katika kuiendesha mbele na kuifanya iwe kubwa kuliko zote duniani.

Yaya Toure
City inaipokea QPR siku ya Jumapili na ikishinda
mechi hiyo wakati Manchester United ikishindwa kushinda Sunderland kwa
angalau mabao kumi basi City itatawazwa bingwa wa msimu wa mwaka
2011/2012.
Alipoulizwa kama ameanza kuhisi shinikizo za
pambano hilo la mwisho, Toure aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa kitita
cha pauni milioni 24, alijibu hapana, kwa sababu nina uzoefu. Nimeisha
shiriki michuano kama hii na kushinda vikombe kadhaa.
Toure, alikua na klabu ya Barcelona iliyoshinda
vikombe sita vya nchini na nje ya nchi mwaka 2009 na amekua kishawishi
kikubwa msimu huu kwa Manchester city.
إرسال تعليق