Kocha msaidizi wa Chelsea Roberto Di Matteo
amehakikishiwa leo kuwa uwamuzi juu ya nafasi yake katika klabu hiyo
utafanywa baada ya fainali ya Klabu bingwa.
Kuna tetesi kuwa Mkufunzi huyo wa muda amekua na
unyonge wa kiasi akihisi kuwa Klabu hiyo ina mipango ya kumpokonya wadhifa
wa kuwa Meneja wake na badala yake wamtafute mtu mwingine, hata ikiwa
matokeo ya mechi dhidi ya Bayern Munich yatakua mazuri.
Lakini
akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa ushirika wa klabu hiyo na timu
ya magari ya mbio za Langalanga ya Sauber, Mkurugenzi mtendaji Ron
Gourlay ameliambia shirika la habari Press Association kuwa, Klabu hiyo
ina imani kubwa na Kocha huyo tangu ajiunge nao kama meneja wa muda na
kwamba watafanya tathmini yao mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, Gourlay alishindwa kujibu kama Di
Matteo amefanya kazi ya kutosha kuwekwa kwenye orodha ya wagombea wa
nafasi ya Meneja wa klabu.
Hata kabla ya kufuzu kushiriki fainali ya Ligi
ya mabingwa, mashabiki wengi walimuunga mkono Di Mateo achaguliwe
kumrithi Andre Villas Boas.
Licha ya imani zote hizo, endapo Di Mateo
atashindwa kuwika mjini Muinich,basi Abramovich ataitumia kama sababu ya
kumuondoa Di Mateo ambaye atakua ameshindwa kuipandisha Chelsea kutoka
nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Premiership na hivyo kukosa
michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya mwakani.

إرسال تعليق