Huu ni mfano wa kuigwa kwa shule zingine
kwani kuwepo kwa mazingira na vifaa vya kufundishia kama vile Kompyuta
kunarahisisha uelewa wa wanafunzi. Safi sana shule ya sekondari Mpunyule.
Shule tatu wilayani Liwale zipo kwenye
mpango wa kusaidiwa kompyuta na shirika lisilokuwa la kiserikali la
UKENGEE FOUNDATION ambalo toka mwaka 2009, limesaidia zaidi ya wanafunzi
9,000 kusoma somo la TEHAMA kwa vitendo tofauti na shule zingine za
serikali ambao husoma nadharia tuu.
Shule ya Sekondari Mpunyule ni shule ya
kata, ina jumla ya kompyuta 20 zinazotumiwa na wanafunzi 264 wa kidato
cha kwanza mpaka cha nne.Kutokana na shule kutokuwa na umeme, kompyuta
hizi zinatumia umeme wa jua. Shule hii ipo kilometa 105 kutoka kilwa
mjini.Hii ni mojawapo ya shule tatu za wilaya ya kilwa zenye vifaa hivi
adimu kwa shule nyingi nchini. Shule zingine zenye kompyuta wilayani
Kilwa ni Kilwa Day na Ilulu.
|
Post a Comment