TANZANIA YAWA NCHI YA KWANZA KUSIGN MAKUBALIANO YA MWONGOZO NA KANUNI ZA UONGOZI KWA WAMILIKI NA MAMENEJA WA VYOMBO VYA HABARI..
:
Waziri
Nchimbi akiweka saini makubaliano hayo na Mwenyekiti wa Moat, Reginald
Mengi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuendeleza Vyombo vya
Habari Afrika (AMI), Amadou Mahtar Ba.
---
TANZANIA
imekuwa nchi ya kwanza Afrika kusaini makubaliano ya mwongozo na kanuni
za uongozi kwa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari.
Mwongozo
huo ulisainiwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki
wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Reginald Mengi na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Mradi wa Mpango wa Vyombo vya Habari (AMI) Amadouh Mahtar Ba.
Kwa
mujibu wa Mengi, lengo la mwongozo huo ni kujenga tasnia ya habari
yenye kuzingatia maadili katika maeneo ya utawala, uwazi na uaminifu
bila kuingiliwa na ushawishi wa mtu yeyote.
Alisema
kumekuwa na wimbo wa maadili ya wanahabari pekee na kusahau suala zima
la wamiliki ambao nao wakati mwingine huchangia kwa kiasi kikubwa habari
kuandikwa ay kurushwa hewani zikiwa na mapungufu ya kimaadili.
Naye
Amadouh alisema kwa mara ya kwanza duniani, kikundi cha wanataaluma ya
habari Afrika kimekutana na kuja na mpango wa kuweka suala la mwongozo
na maadili kwa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari.
Aidha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi
wakati akizindua mwongozo huo, alisema kwa upande wa Serikali inapongeza
mwongozo huo na ina imani utekelezaji wake utafanyika kwa ufanisi kwa
kuwa watekelezaji wake wakuu ndio waanzishili.
Baadhi
ya wadau wa habari waliochangia maoni yao katika mkutano huo ni pamoja
na mwanahabari mwandamizi na mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari
nchini, Jenerali Ulimwengu, Profesa Palamagamba Kabudi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na Kaimu Mhariri Mkuu wa kampuni ya Tanzania Standard
Newspapers (TSN) Mkumbwa Ally.
إرسال تعليق