KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida madiwani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Tarime Mkoani Mara, jana kwa kauli moja waligoma kuendelea na mkutano
wa Baraza la Madiwani wakipinga hatua ya Rais Jakaya Kikwete kumbakiza
katika kituo chake cha kazi mkuu wa wilaya hii, John Henjewele.
Aidha madiwani hao ambao walikutana katika kikao cha kawaida
kilichoitishwa kujadili mbali na mambo mengine taarifa ya Mkaguzi na
Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), walisema hawako tayari kuendelea
na vikao vyovyote katika halmashauri ikiwa Rais Kikwete hatamwondoa
mkuu huyo wa wilaya kwa madai kwamba amekuwa akiendesha utawala wake kwa
ubabe.
Bila kujali itikadi za vyama vyao, madiwani hao 41 walisema watachukua
hatua ya haraka kuwasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara
John Tuppa kumtaka awasilishe ujumbe wake kwa Rais Kikwete wakiomba
kuondolewa haraka wilayani hapo kwa Henjewele.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amos Sagara aliwaambia waandishi wa
habari muda mfupi baada ya kuvunjika kikao hicho kuwa alilalizimika
kuahirisha kikao hicho kutokana na jazba za wazi zilizoonyeshwa na
wawakilishi hao wa wananchi dhidi ya mkuu wa wilaya.
“Sasa katika mazingira kama hayo wameniomba nimuite mkuu wa mkoa
ambaye walisema wanataka kuongea naye kabla ya kuendelea na kikao
chochote nami sikuwa na pingamizi kwa kuwa walidai hawamtaki mkuu wa
wilaya,” alisema.
Alisema kwa kuzingatia uzito wa suala hilo atachukua hatua za haraka
kuwasiliana na mkuu wa mkoa ili kumkutanisha na madiwani kwa kuwa
kisheria hawana mamlaka ya kumuwajibisha DC kutokana na kuwa mteule wa
Rais.
Miongoni mwa tuhuma zilizoainishwa na madiwani hao baada ya kugomea kikao hicho ni..... zaidi ingia hapa:-http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=35788
Post a Comment