Tarime wamkataa DC mpya


 KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, jana kwa kauli moja waligoma kuendelea na mkutano wa Baraza la Madiwani wakipinga hatua ya Rais Jakaya Kikwete kumbakiza katika kituo chake cha kazi mkuu wa wilaya hii, John Henjewele.
Aidha madiwani hao ambao walikutana katika kikao cha kawaida kilichoitishwa kujadili mbali na mambo mengine taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), walisema hawako tayari kuendelea na vikao vyovyote katika halmashauri ikiwa Rais Kikwete hatamwondoa mkuu huyo wa wilaya kwa madai kwamba amekuwa akiendesha utawala wake kwa ubabe.
Bila kujali itikadi za vyama vyao, madiwani hao 41 walisema watachukua hatua ya haraka kuwasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa kumtaka awasilishe ujumbe wake kwa Rais Kikwete wakiomba kuondolewa haraka wilayani hapo kwa Henjewele.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amos Sagara aliwaambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuvunjika kikao hicho kuwa alilalizimika kuahirisha kikao hicho kutokana na jazba za wazi zilizoonyeshwa na wawakilishi hao wa wananchi dhidi ya mkuu wa wilaya.
“Sasa katika mazingira kama hayo wameniomba nimuite mkuu wa mkoa ambaye walisema wanataka kuongea naye kabla ya kuendelea na kikao chochote nami sikuwa na pingamizi kwa kuwa walidai hawamtaki mkuu wa wilaya,” alisema.
Alisema kwa kuzingatia uzito wa suala hilo atachukua hatua za haraka kuwasiliana na mkuu wa mkoa ili kumkutanisha na madiwani kwa kuwa kisheria hawana mamlaka ya kumuwajibisha DC kutokana na kuwa mteule wa Rais.
Miongoni mwa tuhuma zilizoainishwa na madiwani hao baada ya kugomea kikao hicho ni..... zaidi ingia hapa:-http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=35788

Post a Comment

أحدث أقدم