Uamsho wakanusha kuhusika na uchomaji wa kanisa

Katibu
wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh
Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi
akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa
kwao kutolewa kwa vyombo vya habari
Tunatoa wito kwa Jeshi
la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa
kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine
unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza
amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo
haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa
yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kila sifa njema
anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad
(S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.
Jumuia ya UAMSHO
inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa
ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani
vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W)
katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana
mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake
pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya
Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa,
Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.
Jumuia inatoa wito
kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu
wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za
taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda
kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio
yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni
njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na
kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari
kudai nchi yao.
Tunatoa wito kwa
Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama
wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na
vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana
jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za
watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na
kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi na vyombo
vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la
kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za
wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ
Chanzo:- Zanzibar Yetu
إرسال تعليق