Bw. Albert Muchuruzi Mkurugenzi wa kampuni ya Mobile Ticketing Limited
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari
Maelezo wakati walipotambulisha huduma yao mpya ya kuuza tiketi za
mabasi kwa mtandao jijini Dar es salaam, kushoto ni
Costa Kamilija ofisa maendeleo ya biashara, na kulia ni Nancy Mtenga mwakilishi wa kampuni ya mabasi ya Metro.
Costa Kamilija ofisa maendeleo ya biashara, na kulia ni Nancy Mtenga mwakilishi wa kampuni ya mabasi ya Metro.
Afisa maendeleo wa biashara ndg Casta Kamilija akionyesha bango linalo onyesha jinsi ya kununua tiketi kwa mtandao.
Kampuni mpya ya Kitanzania ijulikanayo kama Mobile Ticketing Limited
kwa ushirikiano na Mitandao ya Simu ya Vodacom,Airtel, Zantel na
Makampuni ya Mabasi inayofuraha kuwatangazia kuwa inazindua huduma mpya
na rahisi ya kukata ticket za mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani
kupitia simu ya mkononi. Huduma hii inajulikana kwa Jina la "Ticket popote" ni ya kipekee na ya kwanza kuzinduliwa hapa nchini Tanzania.
Mobile Ticketing Limited
inatambua usumbufu waupatao abilia wakati wanakata kusafiri za mabasi
ya Kwenda Mkoani na Nchi Jirani . Huduma hii inalenga kuondoa utaribu
wa kizamani uliokuwa na usumbufu ambapo abilia alitakiwa kufika kwenye
ofisi za basi husika ili kukata ticket, kuzidishiwa nauli na madalali
(wapiga debe) hasa wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka,
kuuziwa ticket moja mtu zaidi ya mmoja au kuuziwa ticket ya basi
lisilokuwa na safari. Huduma hii mpya ya kukata ticket kwa njia ya
ki”electronic” itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa huu usumbufu,
ambapo abilia ataweza kupata tiketi popote pale alipo, kama atakuwa
anapata mtandao wa simu husika
Chanzo:- Bukoba wadau

إرسال تعليق