Wagombea urais wawili
walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi nchini Misri wametaka
baadhi ya kura zihesabiwe tena, wakidai kulitokea udanganyifu.Wanajeshi hawaruhusiwi kupiga kura Misri.
Msemaji wa Hamdeen Sabahi, kiongozi wa mrengo wa kushoto aliyetokea watatu, alisema kuwa watakata rufaa Jumapili, ili kuzuwia duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Waziri wa zamani wa mashauri ya nchi za nje, Amr Moussa, aliyemaliza wa tano, alimsihi afisa wa mashtaka kufanya uchunguzi.
Kwa matokeo ya hadi sasa, duru ya pili ya uchaguzi itakuwa kati ya Ahmed Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa Hosni Mubarak, na Mohamed Mursi wa chama cha Muslim Brotherhood.
إرسال تعليق