Wakili maarufu afariki Dunia
MKURUGENZI
Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface
Makulilo (44) ‘Jembe’ amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika
Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka
nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia Tanzania Daima jana
asubuhi kutokea kwa kifo hicho ambapo alisema bado ofisi yake na taifa
limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji hilo la uendeshaji wa
mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri
katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa.
Dk.Feleshi
alikuwa akizungumza na gazeti hili kwa uzuni alisema Jumamosi jioni
Boniface ambaye pia alikuwa Msimamizi wa Uendeshaji wa Kesi zenye
maslahi kwa umma, aliingia Dar es Salaam, akitokea Moshi kwaajili ya
kutoa mafunzo ya jinsi ya uendeshaji wa mashitaka kwa maofisa wa Idara
ya Uhamiaji akiwa mwenye afya njema na alirejea nyumbani kwake Kinondoni
lakini ilipofika usiku wa siku hiyo hali yake ilibadilika ghafla na
kukimbizwa katika Hospitali ya Regency kwaajili ya matibabu. “Baada ya
kufikishwa hospitalini hapo alifariki dunia ila mimi kama kiongozi wake
wa kazi kwa sasa siwezi kusema chanzo cha kifo hicho hadi pale
tutakapopata taarifa rasmi za madaktari na msiba upo Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Mtaa wa Sinza Load Kitalu Na.4 na hadi kufikia leo utaratibu
shughuli za msiba zitakuwa zimefahamika na tutawajulisha”alisema
Dk.Feleshi.
Dk.Feleshi
alimuelezea Boniface kuwa ni miongoni mwa mawakili wa serikali
waliokuwa wakijitoa kwa moyo wao wote katika kuitumikia serikali yao
katika uendeshaji wa kesi bila woga na katika kuthibitisha hilo ni
katika kesi za mauji yaliyoibuika miaka ya nyumba mkoani Mbeya ambapo
watu walikuwa wakiwachunya binadamu wenzao ngozi, kesi za wizi wa fedha
za EPA, matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuongeza kuwa marehemu
alikuwa akitumia taaluma yake kwa kuwapatia watu wengine waliokuwa
wakiitaji.
Miongoni
mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia
akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa
nchini sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA,
iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein
ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu
kwenda jela miaka mitano, kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya
shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika
la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda
kesi hiyo mwaka jana, kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara
Jayankumar Patel “Jeetu Patel’ na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne
za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu
kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa,
ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi
hiyo.
Kesi
nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi
umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa
ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya
kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona
mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence
Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo
kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu,
rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro
hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara
ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na
Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja.
Boniface
alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu
shahaha ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria
alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi
mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali
kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa
cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007
alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.
Nyadhifa
ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka
2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya
Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya
Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa
Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri
ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa
wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka
Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma. Bwana alitoa na
bwana ametwaa jina lake liimidiwe.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu, Mei 28 mwaka 2012.

إرسال تعليق