
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Habari
Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk amesema licha ya
fujo ambazo zilitokea May 26 na 27 Usalama umeimarishwa vya kutosha na
kuwataka Watalii waendelee kuja kufanya shuguli zao bila ya woga
wowote.
Amesema Serikali
inabeba jukumu la usalama wa Wageni ambao wanakuja Zanzibar na
kufahamisha kuwa fujo lililotokea halikuathiri Sekta ya Utalii na
maeneo yake muhimu.
Waziri Mbarouk
ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wawakilishi wa Mabalozi
waliopo Nchini kuhusiana na fujo lililotokea jana na juzi kufuatia
kukamatwa kwa kiongozi mmoja wa Jumuiya ya Kidini ya UAMSHO.
Amefahamisha kuwa
maeneo muhimu ya Utalii yakiwemo Mji Mkongwe,Fukwe za bahari na Hoteli
ni sehemu salama ambazo watu wanajishughulisha na kazi zao za kawaida
na kuwaomba Mabalozi hao kuwafahamisha vyema wenzao kile ambacho
kimetokea.
Amesema Jumatatu ya
leo Afisi za Serikali na zile za binafsi ziliweza kufanya kazi ambapo
kwa upande wa wananchi wa kawaida nao waliweza kuendeleza harakati zao
za kila siku kutokana na hali kuwa salama.
Mbarouk ameeleza kuwa
Jeshi la Polisi kwa ufanisi mkubwa liliweza kutuliza vyema fujo za
waandamanaji bila ya kuwepo taarifa yoyote ya kifo au kujeruhiwa kwa
mtu yeyote.
Waziri Mbaruk amesema
kilichotokea ni watu kutumuia uhuru wao wa kidemokrasia wa kuelezea
hisia zao ambazo baadae ziliashiria vitendo vya vurugu jambo ambalo
liliwasababisha Polisi kuchukua hatua za kutuliza vurugu hizo.
Mbarouk amesema
Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inaendelea kuilinda haki ya
kidemokrasia bila ya kutokea vitendo vyoyote vinavyoashiria kuhatarisha
amani Nchini.
Amesema Taarifa ya
Serikali imetolewa Jana na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa
Rais Mohammed Aboud ambayo iliagiza vikosi vyote vya ulinzi kuwa macho
kwa lengo la kutuliza usalama sambamba na kuwakamata wale wote
waliohusika na fujo hizo.
Kwa upande wao
Wawakilishi wa Mabalozi hao walimweleza Waziri huyo kuhakikisha amani
inarudi kama kawaida ili watu waweze kuishi bila ya hofu Mkutano huo
إرسال تعليق