Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye
amezungumzia taarifa zilizo andikwa na baadhi ya Magazeti ya jana
kuhusu kilichosemwa na aliyewahi kuwa waziri wa Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige.
Nape amesema “shutuma alizozitoa Maige, kwanza ikumbukwe kwanza yeye ni Mbunge anaewakilisha Jimbo, juu ya jimbo kuna wilaya na mkoa lakini kama mwanachama ana tawi,Kata na kuna shina ambalo anatoka sasa ukiangalia kwenye level alipo yeye na level nilipo mimi mjumbe wa kamati kuu na katibu mwenyezi wa Taifa wa chama nikianza na mimi kumjibu hadharani nitakua simtendei haki kwa sababu kwakweli sio saizi yangu, naacha vikao vinavyohusika huko chini vishughulike nae na wakifikia mahali wameshindwa basi watatuletea tutashughulika nae”

Gazeti la NIPASHE may 31 2012.
Nnauye
amesema “kuhusu hili swala la kusema wanachama karibu elfu ngapi
wameondoka, ni kwamba CCM ina wanachama wengi sana na hawajaanza leo
kuondoka kutoka CCM, hakuna chama hata kimoja cha Siasa nchini ambacho
kimeanzishwa na wanachama ambao hawakutoka CCM, ukianza mwaka 1992
tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi wanachama wote walioanzisha vyama
vingi walitoka CCM kwa hiyo ni jambo ambalo limefanyika kwa miaka 20 na
CCM haijafa, kwa hiyo leo kuwadanganya wanaccm na Watanzania kwamba
eti kwa sababu kuna watu wawili watatu wamehama kutoka CCM kwenda vyama
vingine CCM inakufa, huu ni uongo wa mchana kweupe”
إرسال تعليق