BARCA YASAJILI KINDA LA MIAKA SITA LA BRAZIL

BARCA YASAJILI KINDA LA MIAKA SITA LA BRAZIL


Camp Nou - Barcelona
Getty
KLABU ya Barcelona imemsajili kinda wa Kibrazil mwenye umri wa miaka sita, Artur Miani mwenye kipaji cha hali ya juu.
Miani alivutia katika majaribio La Masia, Mei mwaka huu, baada ya dada yake kumuandika katika tovuti ya klabu hiyo ya Catalan.
Alipokea barua Ijumaa kutoka Barca ikitangaza kwamba amefuzu majaribio na sasa atakuwa tayari kujiunga na timu ya vijana ya klabu hiyo, Septemba mwaka huu.
"Hii ni baab kubwa," alisema baba yake Artur, Adilson Miani, akizungumza na Globoesporte. "Amekuwa akicheza na watoto wenzake, hajawahi kuonekana katika maisha haya hapo kabla,”aliongeza.

Post a Comment

Previous Post Next Post