BREAKING NEWS; CHOLLO KUTEMWA SIMBA SC

  CHOLLO KUTEMWA SIMBA SC


BEKI wa kulia wa Simba SC, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kipa William Mweta huenda wakatemwa na klabu hiyo, kutokana na ripoti ya daktari wa klabu hiyo, Cossmas Kapinga kusema kwamba wawili hao ni wajeruhi wa muda mrefu.

“Ripoti niliyoiwasilisha kwa uongozi nimesema wazi kuhusu wachezaji hao, kwamba ni majeruhi wa muda mrefu, wanaweza kuwa nje miezi zaidi ya mitatu, ”alisema Kapinga alipozungumza mchana huu.

Katika kutafuta mustakabali wa wachezaji hao, Chanzo:- http://bongostaz.blogspot.com/ ilizungumza na Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Simba, ambaye alisema kwamba uongozi utakutana wakati wowote kuamua hatima ya wachezaji hao na zaidi wanaweza kuondolewa kwenye usajili.

“Hawataachwa moja kwa moja, wataendelea kuhudumiwa na klabu, kila kitu kulingana na mikataba yao, ila wataondolewa kwenye usajili, kwa sababu watakuwa wanajaza nafasi wakati hawawezi kucheza. 

Klabu itawahudumia vizuri, wakipona kama mzunguko wa pili au hata msimu ujao, watarudishwa kikosini,”alisema Mjumbe huyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post