Dogo Janja kurudi kesho Dar kwa ndege kusaini mkataba mnono
Waswahili
wanasema wakati wewe unasema cha nini, wengine wanajiuliza watakipata
lini? Wakati story za Tip Top Connection kuzinguana na Dogo Janja
zinaanza kupungua pole pole kwenye midomo ya watu, magazeti na kwenye
radio, kumeibuka good news kwa mashabiki wake.
Mpaka
unasoma story hii ni kwamba kesho kijana anapanda ndege kurudi Dar es
Salaam baada ya kupigiwa simu na mtu ambaye ameahidi kumsaidia kimuziki
na kumsomesha pia.
Akiongea
na East Africa Radio mchana huu, dogo huyo amesema anakuja kuuangalia
mkataba huo kama ukimridhisha basi atasaini na mambo yaendelee.
Tayari anasema amepata baraka kutoka kwa wazazi wake.
Amewaomba mashabiki wake wampokee airport ili kushow love!
Kila lakheri Dogo Janja.
Source: Leo Tainment
Post a Comment