Familia yaridhia Yondani kwenda Yanga

KAKA yake beki wa Simba, Kelvin Yondani  anayeitwa Sunday Patrick Yondani amesema kwa niaba ya familia ya mzee Yondani wameridhia mchezaji huyo kwenda kuchezea klabu ya Yanga.

Kaka huyo ambaye pia ni wakala wa Yondani ameongeza kuwa ni vyema uongozi wa Simba ukampa baraka na kumwacha mdogo wao afanye kile alichodhamiria kwani anasaka maisha katika umri alio nao.

Kauli ya Sunday imekuja siku moja baada ya klabu za Simba na Yanga kudai mchezaji huyo ni mali yao huku yeye binafsi akisema walishamalizana kimkataba na Simba na yeye yupo huru kusaini kuichezea Yanga katika msimu ujao.

Akizungumza jana kaka huyo wa Yondani alisema kwa niaba ya familia ya mzee Yondani wamekubali  mchezaji huyo kuitumikia klabu ya Yanga baada ya makubaliano ya muda mrefu na tayari amesaini mkataba huku wakitaka uongozi wa Simba kumuacha mchezaji huyo kujitafutia maisha yake.

"Sisi kama familia kwa moyo mmoja tupo na Yondani katika maamuzi yake, jambo la msingi yeye amefuata sheria na hana mkataba wowote na Simba ndio maana hata sisi tumempa baraka za kwenda Yanga, pia viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu kuwa mchezaji huyu bado ni mdogo na anatafuta maisha hivyo wamuache afanye maamuzi yake,"alisema Sunday.

Kwa upande wa beki huyo alisema ni kweli amesaini Yanga na kusisitiza kutaka ushirikiano na umoja ili timu hiyo ifanye vyema katika msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kombe la

Post a Comment

أحدث أقدم