Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Wilson Mukama, amehudhuria
Mkutano wa Vyama rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika uliofanyika
tarehe 8th june 2012 katika hoteli ya Rainbow Tower Hotel, jijini Harare, Zimbabwe.
Mkutano
huo ambao pia umehudhuriwa na Viongozi wa Vyama hivyo rafiki, ambao ni
Makatibu Wakuu wa sasa wa Vyama vilivyopigania Ukombozi Kusini mwa
Afrika ambavyo ni ANC, CCM, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU-PF. Makatibu
Wakuu hao ni komredi Gwede Mantashe, Wilson Mukama, Filipe Paunde,
Juliao Mateus Paulo "Dino Matrosse" na Didymus Mutasa, ambapo kwa Chama
Cha SWAPO kiliwakilishwa na Makamu Katibu Mkuu Komredi Nangolo Mbumba.
Mkutano
huo, ambao ulifunguliwa na Rais wa Zimbabwe ambae pia ni Katibu Mkuu wa
ZANU-PF, Komredi R.G MUGABE, ulitanguliwa na Mikutano ya Wazee,
Wanawake na Vijana wa Vyama hivyo, iliyofanyika tarehe 07 June 2012.
Aidha, Ajenda za mkutano huo zilikuwa ni
(i) Kuanzisha Chuo Cha Pamoja Cha Vyama Hivyo.
(ii) Ripoti juu ya hali za nchi.
(iii) Mikakati ya Ushirikiano katika Chaguzi za Chama.
(iv) Kupitia makubaliano ya Mkutano wa wazee, wanawake pamoja na vijana.
(v) Mipango na Ratiba za Mikutano mwaka 2012-2013.
Pamoja
na mambo mengine umefanya maazimio ya kujenga Chuo cha Siasa katika
eneo la Ihemi, Iringa Nchini Tanzania. Ambapo Chama Cha Mapinduzi
kilipewa jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa taarifa muhimu za ujenzi
ikiwemo ramani na jografia ya eneo husika.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatarajia kurudi Nchini, mwanzoni mwa wiki ijayo.
![]() |
| Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF ambae pia ni Rais wa Zimbabwe. Comrade Robert Mugabe akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano huo. |


إرسال تعليق