Mabao haya ni zawadi kwa mama - Balotelli:

Mario Balotelli scores his secondMSHAMBULIAJI Mario Balotelli amesema kiwango chake kilichoisaidia Italia kuichapa Ujerumani na kutinga fainali ya Euro 2012 ni zawadi kwa mama yake mlezi aitwaye Silvia.Balotelli anayechezea Manchester City ya England alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na kuipa Italia ushindi wa mabao 2-1.

Italia maarufu kama 'Azzurri' sasa itakabiliana na Hispania katika fainali itakayopigwa kesho jijini Kiev.

"Huu ulikuwa usiku wa aina yake katika maisha yangu, natumaini Jumapili itakua zaidi," alisema Balotelli.

Mara baada ya pambano hilo kumalizika, Balotelli aliifuata familia yake iliyokuwa imekaa jukwaa la watu maalumu na kuwakumbatia.
"Mwisho wa mchezo nilikwenda kwa mama yangu, hilo lilikuwa tukio la muhimu zaidi," aliongeza.

"Nilimwambia mama, mabao niliyofunga ni kwaajili yako, kwa muda mrefu nilisubiri tukio la aina hiyo ukizingatia kwamba kwa sasa si mtoto tena naweza kusafiri mbali, hivyo nilitakiwa kuhakikisha anapata furaha, baba yangu pia atakuwa nami katika fainali jijini Kiev."

Mabao hayo mawili ya Balotelli yanamweka katika chati ya wachezaji wanaowania tuzo ya ufungaji bora ya michuano ya Ulaya kwa mwaka  2012 ambapo sasa amefikisha idadi ya mabao matatu.

"Katika soka wakati mwingine unaweza kujaribu mara kadhaa na usifanikiwe na wakati mwingine mara chache tu na ukafanikiwa, nashukuru kwa msaada mkubwa wa Antonio, lakini pasi ya Riccardo Montolivo ilikuwa nzuri zaidi."

Katika mechi hiyo Balotelli alishangilia bao lake la pili kwa kuvua jezi yake na kutunisha misuli. Alisema kitendo hicho hakikukasirika wenzake  kwa sababu nilionyeshwa kadi ya njano, lakini waliona mwili wangu mzuri na kuona wivu,"alitania  baada ya kuulizwa na mwandishi juu ya tukio hilo.

Balotelli ambaye kipindi cha pili kilitolewa alikataa kuwa na majeruhi na kudai yuko fiti kwa fainali Jumapili.

"Kwa kiasi fulani nikuwa nimechoka lakini nilimwambia kocha asubiri dakika tano hata hivyo  wakati huo  tayari uamuzi wa kufanya mabadiliko ulikuwa tayari umefanywa."Italia inashinda ni kwa sababu timu nyingine zinacheza hovyo, nafikiri tulishinda kwa sababu tulikuwa bora hivyo tulistahili.

"Sasa tuna Hispania, sisi sote ni timu bhora katika mashindano haya,"alisema Balotelli na kuongeza:

"Natumaini tutashinda, haijalishi kama tunacheza vibaya ili mradi tunafikia malengo, tunatakiwa kutulia, hatuwezi uchanganyiwa kwakua Hispania wana miliki sana mpira, tunachotakiwa na kucheza mchezo wetu.

"Mpaka wakati huu sisi ndiyo timu pekee iliyoifunga Hispania tulithibitisha hilo kwamba wao na sisi na sawa, hakuna kingine, tunatakiwa kushinda."

Kocha wa Italia Cesare Prandelli alisema kiwango cha Balotelli kimeimarika kama mchezaji wa timu na si yeye binafsi.

"Mario ni wa kipekee, ana nguvu na ana pigana kwaajili ya timu, wakati wote unamwona sehemu mwafaka akipiga eneo la penati," alisema  Prandelli.

Hili itakuwa mara ya pili kwa Italia kukutana na Hispania katika michuano hii, tayari timu hizo zilikutana katika hatua ya makundi na kutoka sare ya bao 1-1.

Post a Comment

Previous Post Next Post