MAN CITY WAMSHUSHA THAMANI VAN PERSIE

MAN CITY WAMSHUSHA THAMANI VAN PERSIE

Van Persie
KLABU ya Manchester City imeghairi kuto zaidi ya pauni Milioni 15 kumsajili Robin van Persie kutoka Arsenal, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo kutoka Goal.com.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu England wameonyesha nia ya kumsajili mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Uholanzi, lakini si kwa dau zaidi ya hilo.






BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba nia ya City kumsajili Van Persie imeshuka baada ya hivi karibuni Arsenal kusema itahitaji zaidi ya pauni Milioni 25 kwa ajili ya mchezaji huyok, ambaye anafikisha miaka 29, Agosti mwaka huu.
Chanzo kimoja cha habari na cha karibu kimesema: “Kiwano hicho hakiwezi kuongezwa na City. Hawako tayari kutoa zaidi ya pauni Milioni 15 ili wampe mshahara mnono.”
City inataka kumpa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki  Van Persie kuhamishia huduma zake Uwanuja wa Etihad.
Hata kama City itafanikiwa kuwauza wachezaji wake Emmanuel Adebayor, Roque Santa Cruz, Wayne Bridge na Kolo Toure kwa dau zuri, lakini bado haitakuwa tayari kumnunua Nahodha wa Arsenal kwa zaidi ya kiasi hicho.
Kocha Roberto Mancini yuko tayari kuachana na mchezaji huyo  na kuhamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Napoli,Edinson Cavani, kama Arsenal haitakuwa tayari kumuuza kwa bei wanayotaka.
Van Persie, ambaye anatarajiwa kwenda kujipumzisha na familia yake baada ya Uholoanzi kutolewa kwenye Euro 2012, amegoma kuongeza mkataba wake Arsenal, ambao unatarajiwa kumalizika mwakani.

Post a Comment

أحدث أقدم