
"Usisikie kwenda kupiga penalti...siku zote sitaki kusikia suala hili, kwani pale ni ufundi tu sasa ukikosea kwa kupiga nje au kumlenga kipa, lawama ndugu yangu" anasema Frank Domayo chipukizi wa JKT Ruvu aliyejiunga na Yanga alipokuwa akiitumikia Taifa Stars Msumbiji.
Domayo alifunga penalti ya saba katika mchezo uliomalizika kwa Stars kufungwa penalti 7-6 na Msumbiji katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini baadaye mwakani. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Taifa Zimpeto jijini Maputo.
"Nililazimishwa kwenda
kupiga penalti baada ya wachezaji wengine kuogopa...mimi siyo mpigaji
mzuri wa penalti kwa hiyo baada ya Boko (John) kupiga penalti ya sita na
kupata na Msumbiji nao wakapiga wakapata, kila mtu aliogopa kwenda
kupiga.
"Ngassa (Mrisho), Samatta (Mbwana) na Haruna (Moshi) wote
walikataa wakanilazimisha mimi kwenda kupiga, nikasema poa tu ngoja
nikajaribu lakini huku miguu ikinitetemeka.
"Wakati ninakwenda
nikawaza, Watanzania wote wananitazama mimi, hizi ndiyo lawama zenyewe
ukikosa. Nilipanga nipige upande wa kulia sikubadili uamuzi, nashukuru
Mungu nilifunga.
"Nikawaangalia Ngassa na Boban...Ngassa akaenda
kupiga penalti ya nane akapata jamaa wakapata, sasa ikabakia kwa Samata
na Haruna wakawa wanasakiziana kwenda kupiga."Mbwana akamwambia Kaseja
piga hiyo, lakini naye akasita basi Samatta akaenda kupiga kwa bahati
mbaya alikosa kwa kipa kuipangua.
"Kaka ile ni presha tupu,
ukisikia mashabiki wanakuzomea wakati unakwenda kupiga penalti unahitaji
umakini na utulivu wa hali ya juu kufanya kile unachotaka," alisema
Domayo.
Waliopata penalti kwa Stars ni Amir Maftah, Shabaan Nditi,
Shomari Kapombe, John Boko, Frank Domayo, Mrisho Ngassa wakati
waliokosa ni Aggrey Morris, Kelvin Yondani na Mbwana Samata.
Lakini
kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesifu uwezo wa kujituma
ulioonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo wao wa juzi dhidi ya
Msumbiji na kusema: "Wachezaji wangu walicheza vizuri na kujituma kama
nialivyotaka.
"Najivunia wachezaji wangu walifanya kile
nilichotaka, lakini bahati haikuwa yao inapofika suala la penalti huwa
hakuna mwenyewe kwani hata timu kubwa Ulaya zinatolewa.
"Jambo
zuri zaidi ni kwamba tumekuja hapa na kufunga mabao kama tulivyowahidi
wa Tanzania, kwamba tunakwenda Msumbiji tutapata bao ndicho tulichofanya
tena tumepata mabao saba.
Kim aliwapongeza wenyeji kwa kutumia vizuri nafasi yao ya kuwa nyumbani na kupata ushindi huo.
Naye nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema bahati haikuwa yao, lakini sasa ni wakati wa kujipanga upya.
"Timu ni nzuri, tumecheza mechi nne sare moja na Malawi, tukafungwa na Ivory Coast na tumeshinda Gambia kabla ya kufungwa Msumbiji. Nadhani wote mmeona mabadiliko."
Naye nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema bahati haikuwa yao, lakini sasa ni wakati wa kujipanga upya.
"Timu ni nzuri, tumecheza mechi nne sare moja na Malawi, tukafungwa na Ivory Coast na tumeshinda Gambia kabla ya kufungwa Msumbiji. Nadhani wote mmeona mabadiliko."
"Watanzania wanatakiwa kuwa na subira ili timu
iendelee kujiamini kwa sababu kuna wachezaji wengi ni chipukizi na
wengi wanacheza vizuri," alisema Kaseja. Naye beki Kelvin Yondan alisifu
jinsi walivyojituma na hata kusawazisha bao japokuwa wametolewa kwa
mikwaju ya penalti.
إرسال تعليق