PNC: Nina bifu na maisha na si wasanii wenzangu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na kibao chake cha
Aiyolela, Pancras Ndaki Charles ‘PNC’ amesema ana ‘bifu’ na maisha na si
wasanii wenzake kama watu wengi wanavyodai.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, PNC alisema, amekuwa akisikia
maneno mtaani kuwa, ana ugomvi na msanii mmoja maarufu hapa nchini
kutokana na kukwaruzana naye, kisa uwezo wa kutunga nyimbo zenye
mashairi ya mvuto kwa mashabiki.
“Nina bifu na maisha na si wasanii wenzangu. Ninachopigania ni kuona
nakuwa na maisha mazuri siku zijazo, ndiyo maana naumiza kichwa
kuhakikisha natoa vibao ambavyo vina mvuto kwa mashabiki wangu na si
kulumbana na wasanii wenzangu,” alisema PNC.
Msanii huyo aliye chini ya ‘lebo’ ya Mtanashati Entertainment alisema
kuwa, katika maisha yake hapendi kugombana na wasanii wenzake, kwani
kufanya hivyo ni kuendelea kujiwekea maadui wasio na faida katika maisha
yake.
Mbali na kibao cha ‘Aiyolela’, msanii huyo ameachia wimbo mwingine
unaokwenda kwa jina la ‘Binadamu’ ambao nao umeonekana kuwashika wadau
wa muziki wa kizazi kipya.
Post a Comment