PNC: Nina bifu na maisha na si wasanii wenzangu

PNC: Nina bifu na maisha na si wasanii wenzangu


MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na kibao chake cha Aiyolela, Pancras Ndaki Charles ‘PNC’ amesema ana ‘bifu’ na maisha na si wasanii wenzake kama watu wengi wanavyodai.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, PNC alisema, amekuwa akisikia maneno mtaani kuwa, ana ugomvi na msanii mmoja maarufu hapa nchini kutokana na kukwaruzana naye, kisa uwezo wa kutunga nyimbo zenye mashairi ya mvuto kwa mashabiki.
“Nina bifu na maisha na si wasanii wenzangu. Ninachopigania ni kuona nakuwa na maisha mazuri siku zijazo, ndiyo maana naumiza kichwa kuhakikisha natoa vibao ambavyo vina mvuto kwa mashabiki wangu na si kulumbana na wasanii wenzangu,” alisema PNC.
Msanii huyo aliye chini ya ‘lebo’ ya Mtanashati Entertainment alisema kuwa, katika maisha yake hapendi kugombana na wasanii wenzake, kwani kufanya hivyo ni kuendelea kujiwekea maadui wasio na faida katika maisha yake.
Mbali na kibao cha ‘Aiyolela’, msanii huyo ameachia wimbo mwingine unaokwenda kwa jina la ‘Binadamu’ ambao nao umeonekana kuwashika wadau wa muziki wa kizazi kipya.

Post a Comment

أحدث أقدم