
Ushindi wa Czech umewaondoa wenyeji Poland
NYOTA wa Jamhuri ya Czech, Petr Jiracek alifunga bao la pekee katika
mechi ya uwanja wa Wroclaw dhidi ya wenyeji Poland siku ya Jumamosi, na
kuwahuzunisha mashabiki wa nyumbani, wakati Jamhuri ya Czech ilipofuzu
kuingia robo fainali za mashindano ya Euro 2012.
Jamhuri ya Czech imefuzu katika kundi hilo, baada ya kuongoza kwa pointi 6.
Jiracek, kiungo cha kati wa timu ya Wolfsburg ya Ujerumani, aliweza
kuutambariza mpira wavuni katika sehemu ambayo kipa Przemyslaw Tyton
hakuweza kuwa na matumaini kabisa ya kuufikia mpira, zikiwa zimesalia
dakika 18 tu mechi hiyo kumalizika.
Poland walianza mechi wakifahamu kwamba iwapo wangelipata ushindi katika
mechi hiyo, basi wangeliweza, kwa mara ya kuwanza, kuwa miongoni mwa
timu nane ambazo zingelisalia katika mashindano kushiriki katika mechi
za robo fainali.
Nahodha wa Poland Jakub Blaszczykowski, katika juhudi za dakika ya
mwisho alikuwa nusra afunga bao la kusawazisha, lakini ulinzi wa Czech
ulikuwa thabiti, na mpira kuondolewa kabla ya kuvuka msitari.
Post a Comment