Polisi walipua mabomu kudhibiti wananchi

 Polisi walipua mabomu kudhibiti wananchi

VURUGU kubwa zimezuka katika Mji wa Buhemba, Musoma Mkoani Mara na polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliotaka kuchoma moto kituo kidogo cha polisi Buhemba.

Wananchi hao walichukua hatua hiyo wakiwatuhumu polisi kushirikiana na majambazi kuvamia wanunuzi wa dhahabu katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba na kuua watano kati yao na kujeruhi wengine watano.

Watuhumiwa hao wa ujambazi walivamia mji huo juzi majira ya saa 9 alasiri, wakiwa na silaha za moto na mapanga ndipo wapolifanikiwa kuchukua pesa na madini waliyokuwa nayo wafanyabiashara hao huku wakifanya mauaji hayo kwa kutumia risasi na kuwacharanga kwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao.

Kufuatia mauaji hayo yaliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma wananchi wa Buhemba walipatwa na simanzi na jazba,  hilo ambalo usiku wa kuamkia jana wananchi hao walijikusanya na kupanga maandamano hadi katika kituo kidogo cha polisi Buhemba kwa lengo la kukichoma moto.

Wananchi hao walidai kwamba kwa madai kuwa Polisi wa kituo hicho walishirikina na majambazi hao kwa kuwalinda hali iliyopelekea kutokea kwa mauaji hayo ya kinyama.

Habari zaidi zilisema pamoja na wananchi kutoa taarifa polisi muda mfupi baada ya majambazi hao kuvamia Buhemba, polisi walichukua zaidi ya saa tatu kufika eneo la tukio na hivyo kukuta majambazi hayo yameshkimbia.

Kufuatia kitendo hicho cha polisi kuchelewa kufika, wananchi ndipo walipopandwa na hasira na jana kuzingira kituo hicho, lakini idadi kubwa ya polisi kutoka Musoma mjini walipelekwa katika eneo la tukio ambako walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wenye hasiara walioandamana na kutaka kuchoma moto kituo kodogo cha polisi Buhemba.

Wakazi hao walitaka kukichoma kituo hicho kwa madai kuwa polisi wanashirikiana na majambazi hasa baada ya juzi kushindwa kufika katika eneo la tukio kwa wakati jambo lililosababisha mauji hayo kutokea.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Peter Mguzu alisema polisi waliposikia habari ya wananchi kuchoma kituo cha polisi walifika haraka eneo la tukio wakiongozana na kamanda na Mkuu wa Mkoa huo, John Tupa wakati siku ya tukio walichelewa na kushindwa kuokoa maisha ya watu.

“Nashangaa leo (jana) wamefika haraka kwenye eneo la tukio baada ya kusikia kuwa wananchi wanataka kuchoma kituo cha polisi, lakini jana (juzi) wakati majambazi yanavamia walionekana kupuuza taarifa tulizowapa,” alisema Mguzu.

Baada ya vurugu hizo kutulia jana jioni Kamanda Mwakyoma aliitisha mkutano wa dharura na wananchi hao ili kupata suluhu ya madai ya wananchi hao ambayo ni pamoja na kuondolewa kwa polisi wa kituo cha Buhemba wanaodai kukumbatia vitendo viovu kijijini hapo.

Post a Comment

أحدث أقدم