SHIRIKA LA NDEGE LA DANA LAPOKONYWA LESENI

Mabaki ya ndege ya shirika la Dana
Mamlaka
ya safari za ndege nchini Nigeria, imelipokonya leseni ya biashara ya
shirika la ndege linalomiliki ndege iliyoanguka mjini Lagos siku ya
Jumapili na kusababisha vifo vya watu 150.
Mamlaka
hiyo ilisema kuwa shirika la ndege la Dana Air, halitaendesha safari
zake za ndege tena hadi itakapochunguzwa kikamilifu.
Jamaa
za waliofariki kwenye ndege hiyo wanajaribu kutambua miili za jamaa wao
ambayo iko kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Lagos.
Afisaa
mmoja wa mamlaka hiyo, alisema kuwa rubani alikuwa ameelezea kuwa ndege
ilikuwa na matatizo ya kiufundi kwenye injini zake mbili, kabla ya
ndege hiyo kuanguka.
Chanzo - BBC Swahili
إرسال تعليق