Edo Kumwembe, AbidjanMPELELEZI wa vipaji vya soka toka klabu tajiri England, Manchester City, Joe Mulberry alitua kwa siri mjini Abidjan na kupiga kambi kwenye hoteli ya Ibis Plateau, ambayo pia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilifikia na lengo lilikuwa moja tu kuwachunguza wachezaji wa timu hiyo, Mwananchi limebaini.
Mulberry, raia wa Uingereza mwenye jukumu la
kuchunguza vipaji kwa nchi za Afrika Magharibi, alifanya kazi ya
kuipeleleza Stars bila kutaka mtu yeyote kufahamu kabla ya mwandishi wa
habari hizi kumbaini.
Awali, Mulberry aliyeweka makazi yake nchini Ghana alipanga kwenye chumba namba 604 cha hoteli ya Ibis Plateau.
Baada
ya gazeti hili kupata fursa ya kuongea naye muda mrefu, lilimbaini na
ndipo naye alipomfichua siri kwamba alikuja Abidjan kwa ajili ya
kuangalia pambano la Stars dhidi ya Ivory Coast.
Kwa mujibu wa
uchunguzi wake wa haraka, Mulberry alivutiwa na kipaji cha mshambuliaji
Mbwana Samata na cha kushangaza katika kipindi kifupi tayari alikuwa
amekusanya habari zote za Samata.
Miongoni mwa dodoso muhimu
alizokusanya ni pamoja na mabao mawili aliyofunga wakati wa mchezo wa
Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Dynamo ya Zambia na El Merreikh ya
Sudan akiwa na timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Mulberry alikiri Samata alikuwa na kipaji kikubwa lakini
akataka amuone zaidi siku za usoni kujua kama alikuwa na uwezo mkubwa wa
kufunga kama ilivyo katika kuuchezea mpira.
“Nitasafiri kwenda
Ghana kumtazama kwa ajili ya pambano la ligi ya mabingwa kati ya Berekum
Chelsea dhidi ya TP Mazembe pale Accra, Julai 5. Kama atakuwa yuko safi
tena nitajaribu kuzungumza na timu yake.”
Hata hivyo, Mulberry alisema Samata hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sasa na badala yake anaweza kupelekwa katika ligi nyingine kabla ya kupata uzoefu wa kucheza ligi kubwa Ulaya.
Hata hivyo, Mulberry alisema Samata hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sasa na badala yake anaweza kupelekwa katika ligi nyingine kabla ya kupata uzoefu wa kucheza ligi kubwa Ulaya.
Wakati huohuo, msafara Taifa
Stars, unatarajiwa kuwasili leo asubuhi na ndege ya Shirika la ndege la
Kenya Airways ukitokea mjini Abidjan ilipocheza na kufungwa na wenyeji
wao, Ivory Coast kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali
za Kombe la Dunia.
Stars ilitarajiwa kuondoka Abidjan jana usiku
na kupitia Nairobi usiku wa manane kabla ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa moja asubuhi leo.
Kabla
ya kuondoka Abidjan, kocha wa taifa Stars alikuwa ameendeleza programu
yake ya mazoezi kama kawaida, huku akiwataka wachezaji wa timu hiyo
wasizembee katika pambano la Jumapili dhidi ya Gambia.
Mchezaji
pekee ambaye alikosekana katika mazoezi ya juzi na jana alikuwa ni
mlinzi wa kushoto wa timu hiyo, Waziri Salum ambaye aliumizwa kwa bahati
mbaya kifundo chake cha mguu na mlinzi mwenzake, Erasto Nyoni
Chanzo:- Mwananchi
إرسال تعليق