fKLABU ya Simba imeanza harakati za kuimarisha kikosi cha msimu
ujao kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa kwa kusajili nyota
ambao watakuwa tishio.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimedokeza kuwa, chini ya mkakati
huo, Simba imeanza harakati za chinichini za kufuatilia nyendo za
wachezaji wa ndani na nje ya nchi.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba, kilidokeza jana
kuwa, kwa sasa klabu hiyo imo kwenye harakati za kumsajili mchezaji
kutoka Sofapaka ya Kenya.
Tayari viongozi wawili wa klabu hiyo, wapo nchini Kenya kumfuatilia
mchezaji huyo ambaye jina lake kwa sasa, wametaka liwe siri kwani mambo
hayajakamilika.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Ibrahim Masoud, jana
walikuwa Nairobi, Kenya kuweka mipango sawa.
Chanzo hicho kilisema kuwa, kilichowapeleka si kuchunguza uwezo wa
nyota huyo, kwani walishamfuatilia kwa muda mrefu na kujiridhisha kuwa,
atakuwa ni nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya timu hiyo kwa mujibu wa
matakwa ya Kocha Milovan Cirkovic.
Simba wamekuwa katika juhudi za kusaka wachezaji wa kuimarisha kikosi
chao, na tayari ina wageni wawili; Musa Muse (Uganda) na Patric
Mbiyavamba (DR Congo) wanaofanyiwa majaribio.
Simba ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania bara,
wanakabiliwa na michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika baadaye mwezi
huu, Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
إرسال تعليق