
MIchel Platini
RAIS wa Shirikisho la Soka Ulaya, (UEFA) Michel Platini anasema njia
bora ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka ni kwa
waamuzi kusimamisha mechi wakati inabainika kuna ubaguzi huo.
Wiki iliopita kipindi cha BBC cha Panorama kilionyesha matukio ya
ubaguzi wa rangi katika viwanja vya Poland na Ukraine, wenyeji wa
mashindano ya mataifa bingwa barani Ulaya mwaka 2012, yanayoanza siku ya
Ijumaa.
" Muamuzi anaweza akamaliza mechi. Sasa wana uwezo huo wakati suala la
ubaguzi wa rangi linapojitokeza," alimwambia mhariri wa michezo wa BBC
David Bond.
" Nafkiri, hiyo ndiyo njia nzuri ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika mchezo huu."
Platini alikanusha taarifa kuwa hadhi yake itashuka kama kutatokea
matukio ya ubaguzi wa rangi katika mashindano ya mwaka huu 2012.
" Hadhi yangu, kwa kuwa kuna wabaguzi wa rangi nchini Poland na Ukraine -
unafanya mzaha? Unafkiri ni jukumu langu kwa wabaguzi wote wa rangi
barani Ulaya au England au Ufaransa?" alisema.
" Jukumu langu ni kukabiliana na tatizo hilo - na nimejitahidi
kubadilisha sheria, kubadilisha kanuni, kusaidia kwa kauli mbiu ' Watu
wote ni sawa' na ' Isifanyike Tena'. Tunawasaidia sana, tunafanya mengi
kukabiliana na ubaguzi wa rangi - lakini si jukumu langu kwa jamii
nzima.
إرسال تعليق