Terry anaokoa bao la wazi
BAO pekee la Wayne Rooney lilitosha kumfanya awe shujaa tena England
wakati ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ukraine na kuongoza Kundi D
sambamba na kuingia Robo Fainali ya Euro 2012 ambako watamenyana na
Italia.
Mshambuliaji huyo alifunga akiunganisha krosi ya Nahodha Steven Gerrad iliyopanguliwa na kipa Andriy Pyatov .
Pamoja na hayo,
ilipoteza nafasi kibao na bao la wazi zaidi alikosa Marko Devic ambaye
shuti lake lilionekana kuvuka mstari, kabla ya Terry kuosha na refa
hakutoa bao.
Sweden
iliyoifunga 2-0 Ufaransa, mabao ya Ibrahimovic dakika ya 54 na Larsson
dakika ya 90, imeihakikishia England kufuzu kama kinara wa kundi hilo.
|
Post a Comment