ROONEY AIPELEKA ENGLAND ROBO FAINALI KIFUA MBELE

ROONEY AIPELEKA ENGLAND ROBO FAINALI KIFUA MBELE, UFARANSA YAPIGWA 2 - 0 UZY

Rooney anafunga

John Terry anampongeza Rooney
Ibra anawafunga Ufaransa

Terry anaokoa bao la wazi
BAO pekee la Wayne Rooney lilitosha kumfanya awe shujaa tena England wakati ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ukraine na kuongoza Kundi D sambamba na kuingia Robo Fainali ya Euro 2012 ambako watamenyana na Italia.
Mshambuliaji huyo alifunga akiunganisha krosi ya Nahodha Steven Gerrad iliyopanguliwa na kipa Andriy Pyatov .
Pamoja na hayo, ilipoteza nafasi kibao na bao la wazi zaidi alikosa Marko Devic ambaye shuti lake lilionekana kuvuka mstari, kabla ya Terry kuosha na refa hakutoa bao.
Sweden iliyoifunga 2-0 Ufaransa, mabao ya Ibrahimovic dakika ya 54 na Larsson dakika ya 90, imeihakikishia England kufuzu kama kinara wa kundi hilo.

Post a Comment

أحدث أقدم