MWANZO HADI MWISHO WA MH. MNYIKA KUTOLEWA NDANI YA BUNGE.

 Mh. John Mnyika alipokuwa akitoa maoni na kuchangia Bajeti wakati wa kipindi cha maswali na majibu nakujikuta akiamuriwa kutoka nje Baada ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Rais na Wabunge wa Chama cha Mapinduzi alipotakiwa kurekebisha kauli yake.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA Mh. John Mnyika akitoka Bungeni baada ya Naibu Spika Job Ndugai kumuamuru atoke kbaada ya kushindwa kufuta kauli yake ya kumuita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni dhaifu.
Mh. John Mnyika akisindikizwa na Askari wa Bunge ambao waliamuriwa na Naibu Spika kutoka nje ya Bunge.
Mbunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Mh. John Mnyika akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutolewa Bungeni.
Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo wakibaki na butwaa baada ya kumuona Mh. Mnyika akiondoka kwa jazba na kupakia taxi.
UFUATAO NI MSIMAMO WA MH. MNYIKA ALIOANDIKIA KWENYE BLOG YAKE
Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!
John Mnyika
19 Juni 2012

Post a Comment

أحدث أقدم