URENO YAPIGWA KIDUDE NAYO, RONALDO AFUNIKWA
LVIV, Ukraine
BAO pekee la Mario Gomez lilitosha
kuipa Ujerumani ushindi wa 1-0 usiku huu dhidi ya Ureno katika mechi ya
Kundi B ya Kombe la mataifa ya Ulaya mjini hapa.
Gomez alifunga bao hilo, muda mfupi baada ya kumpisha uwanjani Miroslav Klose, ambaye alikuwa tayari kwenye mstari wa kuingia uwanjani, wakati anaiwahi krosi ya Sami Khedira dakika ya 72 na kuitupia nyavuni.
![]() |
| Gomez |
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alichelewa
kufanya mabadiliko hayo baada ya bao hilo na Gomez alikaribia kufunga
bao lingine kabla ya kutolewa dakika ya 80 akicheza siku ambayo
anasherehekea miaka 34 ya kuzaliwa kwake.
Nani
aligongesha mwamba dakika ya 84th, ikiwa ni mara ya pili Ureno kufanya
hivyo kwenye lango la wapinzani wao hao. Shuti la Silvestre Varela
lilikwenda moja kwa moja kwa kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer dakika ya 89.
Ujerumani
walitawala mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa, Pepe alipata nafasi
nzuri kipindi cha kwanza, na mpira mwamba wa chini wa lango la Ujerumani
wakati akiujaribu kuunganisha kona kabla ya mpira kutoka nje.
Licha ya kusema kabla ya mechi hiyo kwamba atawaanzisha mkongwe Klose kama mshambuliaji, Loew alimtanguliza Gomez.
Katika hatua nyingine ambayo haikutarajiwa, Loew pia alimchezesha Mats Hummels katika beki ya kati badala ya Per Mertesacker.
Mertesacker na
Klose wameingia kwenye michuano hiyo baada ya kuwa majeruhi kwa muda
mrefu. Mertesacker alicheza mechi mbili tu za kirafiki baada ya
kufanyiwa upasuaji Februari, mwaka huu na Klose pia alicheza kidogo
baada ya kuumia Machi. Mshambuliaji huyo pia alilalamikia maumivu ya
mgongo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Jerome Boateng alicheza beki ya kulia na pia Loew amesikitishwa na habari za magazeti kuhusu maisha yake ya usiku.
IMwishoni,
ilidhihirika uamuzi wa Loew ulikuwa sahihi. Hummels alicheza vizuri,
Boateng alifanya kazi nzuri ya kumdhibiti Cristiano Ronaldo na Gomez
alifunga bao muhimu.



إرسال تعليق