Wanaobashiriwa kulimwa kadi nyekundu

WARSAW, Poland
FAINALI za Mataifa ya Ulaya zilizoanza mwishoni mwa wiki iliyopita, zimekuwa zikibashiriwa kwa mitazamo mbalimbali.

Katika fainali hizo, kuna wachezaji ambao wanashindwa kutofautisha mechi za ligi na Fainali hizo kwani ni tofauti na walivyozoea kucheza. Kati ya waliobashiriwa kulimwa kadi nyekundi, kipa wa Poland, Wojciech Szczesny hakuwemo japo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kwanza kupata kadi.

Nani ambaye anatarajiwa kupata kadi nyekundu? Kutokana na rekodi za wachezaji, mtandao wa Goal.com umeangalia aina ya wachezaji.

5: PEPE
Ni beki wa kati wa Real Madrid, pamoja na mchezaji mwenzake Sergio Ramos. wachezaji hawa wana kadi kati ya 10 na 12 katika ligi ya Hispania, na kadi nyekundu moja kwa kila mmoja, lakini Pepe ni mara yake ya pili kwa kila msimu.

Wachezaji wenzake wa Ureno wanatakiwa kuwa na mtazamo mwingine wa kutowaamini sana hasa Sergio Ramos wakati Pepe kupata kadi nyekundu ni jambo la kawaida na ni wakati wowote.
 
Mwingine ni mchezaji wa Getafe’, Francisco Casquero anayeweza kuelezea undani wa Pepe kuwa aliwahi kucheza rafu ndani ya 18 na kusababisha penalti, japokuwa mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

4: SOKRATIS PAPASTATHOPOULOS
Ni beki ya Ugiriki inayocheza kazi katika kikosi cha Otto Rehhagelna alikuwa kwenye kikosi cha ubingwa wa Euro 2004, na aliruhusu mabao matano.

Katika ngome hiyo, Sokratis Papastathopoulous ni wazi anabashiriwa ni kati ya wachezaji wanaoweza kulimwa kadi nyekundu kirahisi. (Tayari ameonyeshwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Poland)

Beki huyo anayekipiga, Werder Bremen alikusanya kadi 13 za njano katika mechi zake 30 za Bundesliga msimu huu. Licha ya kupata nyekundu moja, haonekani kama mchezaji mwenye busara uwanjani.

3: NIGEL DE JONG
Ni Eric Cantona ndiye anaweza kufananishwa na Nigel De Jong. Mchezaji huyu ndiye aliyempiga kiatu cha kifua, Xabi Alonso katika Fainali za Kombe la Dunia 2010.

Hata hivyo, hakuonyeshwa kadi nyekundu, De Jong aliwahi kupata kadi moja nyekundu katika maisha yake ya soka. Kwa kuwa anapata namba kwa msimu katika kikosi cha Manchester City ilikuwa ngumu kutambua nidhamu yake sawasawa.

Kingine ambacho kinamfunga mchezaji huyo wa Uholanzi ni pale alipomkwatua kwa makusudi Hatim Ben Arfa katika mechi za Ligi Kuu ya England.

2: JOHN TERRY
Nahodha wa Chelsea alikosa mechi ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, baada ya kumkwatua kwa makusudi beki wa Barcelona,  Alexis Sanchez katika nusu fainali. Hadi kumalizika kwa msimu, Terry alikusanya kadi nane za njano.

Terry anafananishwa na Anton Ferdinand katika kikosi cha England lakini Rio Ferdinand naye angeweza kufananishwa kidogo kwani anaonyesha nidhamu kuwepo. Terry ni kati ya wachezaji wanaokubalika lakini wasio na nidhamu.

1: MARIO BALOTELLI
Katika kikosi cha Italia, Mario Balotelli atakuwa na kazi ya kumpa presha kocha wake,  Cesare Prandelli, kutokana na aina ya soka yake ya utata.

Balotelli mmoja wa wachezaji matata wa Manchester City, itakumbukwa aliondolewa kwa kadi nyekundu mechi ya Arsenal kwa kumkwatua kwa makusudi Bacary Sagna, na alimuumiza Alex Song kipindi cha kwanza, lakini hakuadhibiwa.

Mapema Januari, alifungiwa mechi nne na FA kwa kumpiga buti, Scott Parker wa Tottenham waliposhinda 3-2 kwenye Uwanja wa Etihad, na Novemba mwaka jana, alilimwa kadi mbili za njano dhidi ya Liverpool.

Post a Comment

Previous Post Next Post