XAVI AVUNJA REKODI YA PASI ULAYA

XAVI AVUNJA REKODI YA PASI ULAYA


Xavi Hernández - Spain
Xavi

KIUNGO wa Hispania, Xavi amevunja rekodi ya kugawa pasi katika Kombe la Mataifa ya Ulaya usiku huu, akiiongoza timu yake kushinda 4-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
Kiungo huyo mchezeshaji alitoa mapande 136 usiku wa Alhamisi na kati ya hizo pasi 127 zilifika kwa walengwa. Rekodi ya awali ya pasi 117 iliwekwa na gwiji wa Uholanzi, Ronald Koeman, ambaye alifanya mavitu hayo katika michuano ya mwaka 1992 dhidi Denmark.
Hispania pia iliweka rekodi katika michuano ya Ulaya, kutokana na kugonga pasi 860 dhidi ya Vijana wa Kijani.
La Roja walikisambaratisha kikosi cha Giovanni Trapattoni 4-0 huku wakitawala mchezo kwa asilimia 78.
Sasa wanaongoza Kundi C sambamba na Croatia, ambao watamenyana nao katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Jumatatu.

Post a Comment

أحدث أقدم