ZANZIBAR WAREJEA NA SHABA, WAUA 7-2 MECHI YA MWISHO

ZANZIBAR WAREJEA NA SHABA, WAUA 7-2 MECHI YA MWISHO


Wachezaji wa Zanzibar Heroes

TIMU ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imerejea nchini jana ikitokea Uzbekistan ilikokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Dunia ya VIVA, inayohusisha nchi ambazo si wanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na kuambulia Medali ya Shaba.
Zanzibar ilishinda Medali hiyo, baada ya Jumapili kuifunga Province ya Ufaransa mabao 7-2 katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.
Awali, katika mchezo wa Nusu Fainali, Zanzibar ilifungwa mabao 2-0 na Cyprus na Kaskazini, hivyo kukosa tiketi ya kucheza Fainali.
Katika mechi za Kundi lake A, Zanzibar ilifanikiwa kutinga Nusu Fainali baada ya kuzifunga Ratia 6-0 na Elaam 3-0.
Wachezaji wa Zanzibar sasa watarejea kwenye klabu zao, kabla ya kuitwa tena baadaye kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Challenge, ambayo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka.

Post a Comment

أحدث أقدم