AIRTEL WAZINDUA KITU CHA DAKA SALIO
![]() |
| Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (katikati) akizungumzia promosheni mpya ya Daka Salio, leo makao makuu ya Airtel, Morocco, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Salim Madati Meneja Huduma za Ziada Airtel na kushoto Dangio Kaniki, Ofisa Mahusiano wa Airtel Tanzania. (Habari kwa hisani ya:- http://bongostaz.blogspot.com/ |
![]() | ||
|
![]() |
| Hamad Michuzi wa Jiachie Blog, akipandisha vitu fasta baada ya kuchukua habari za promosheni mpya ya Airtel Tanzania. Daka Salio. Kushoto kwake Mwakibete wa Mo Blog. |
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel kwa kuendeleza dhamira yao ya Uhuru wa kuongea imetoa fulsa nyingine kwa
wateja wake kwa kuzindua huduma kabambe ya Daka salio ikiwa ni jitihada zake
katika kutimiza dhamira yake ya kuendelea kutoa uhuru wa kuongea kwa wateja
wake nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando by Jackson Mmbando alisema
“Airtel tumeamua kuleta huduma hii ya Daka salio kwa wateja wetu wote
waendelee kufurahia huduma zetu kila wakati, ikiwa sasa unaweza kukopa na
kuongea na ndugu au rafiki wa mtandao wowote sasa hakunakubeep tena
Hii ni huduma nzuri kwa
familia, marafiki ndugu au jamaa kwa kuwa itaondoa tatizo la watu kubeep,
Airtel tunasema kwanini ubeep au uteseke kukopa kiwango kikubwa na kulipa
zaidi. Daka salio kidogo na ulipie kidogo na airtel. Ili kufurahia huduma
hii ni rahisi na haraka tuma tu neno daka kwenda 15549. Uongee mwanzo
mwisho, kwa raha zako.
Mteja yeyote anaweza kukopa
ikiwa tu amekuwa mteja wa Airtel kwa mfululizosiku tisini, awe anasalio la hadi
shilingi 50 na asiwe anadaiwa deni la Daka salio ikiwa alishakopa kupitia
huduma hii
Faida ya kukopa salio ya
Airtel ni kwamba tunakukopesha kiwango kidogo ambacho utalipia kiduchu tu na
utaongea kwa muda mrefu. Achana na wanaokopesha kiwango kikubwa halafu unaongea
kidogo.
Mteja wa Airtel anaekopa
salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na akitaka kulipa atalipa ziada ya
sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu, kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500
bado utabakia na salio la kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel
Airtel imekuwa na
ubunifu wa bidhaa na huduma zake zaidi kwa lengo la kufaidisha jamii kwa
ujumla. Hivi karibuni ilizindua huduma ya SUPA 5 yenye dili tano bomba na
inaendelea kutoa unafuu kwa wateja wa Airtel kupata sms 200 bure, kuongea na
watu watatu kwa nusu shilingi siku nzima, kupata huduma ya facebook bure
, intaneti bure usiku, pamoja na kongea kwa robo shilingi nyakati za usiku kwa
kupiga tu *149*99# na kufuata utaratibu
Airtel pia kupitia huduma
yake ya Airtel money inawawezesha wajasiliamali waliowekeza katika kwa kuwa
wakala wake nchi nzima pamoja na wateja wake, kwa wateja sasa
wanapata mara mbili ya salio wanaloongeza kupitia huduma ya Airtel
Moneywakati WAKALA wote nchi nzima watapata mara mbili ya kamisheni zao
kwa mwezi juni - julai kwa mihamala yote watakayofanya kupitia Airtel Money.




Post a Comment